Kuna Tetesi ambazo ziko mtaani na zinasambaa kwa chini chini kuwa msanii ambaye yuko chini ya Uongozi wa Tanzania House of Talent ( THT) Amini Amejitoa kwenye nyumba Hiyo ya vipaji. Chanzo chetu cha habari kinahabrisha kuwa msanii amini alisimamishwa na uongozi wa nyumba hiyo ya vipaji hivi karibu.

GongaMx ilijaribu kumtafuta Amini kwa Njia ya simu na amini alifunguka kwa kusema kuwa ni mapema kulizingumzia hilo cos yuko kwenye maandalizi ya kuzindua na kutoa single yake mpya itakayokwenda kwa jina la ni Wewe. na kuhusu yeye na uongozi wake wa THT bado mapema kulizingumzia na wakati utakapofika kila kitu kitawekwa wazi.

Kumbuka amini ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa THT, ambaye alishawahi kuwatungia wasanii mbalimbali wa kundi hilo akiwemo Mwasiti na wengine kuwapa ushauri na hata kuwasaidia katika kutafuta sauti ya wimbo.

Pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamuziki mwenzake wa kundi hilo Linah.

Swali watu bado wanajiuliza juu ya kuhama kwake THT, ni kweli? Kwa nini? Wapi anatarajia kwenda?

 

 

 

Views: 162

Comment

You need to be a member of GongaMx to add comments!

Join GongaMx


follow us on

Badge

Loading…

© 2012   Created by GongaMx.

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service